Timu yafanya mazoezi ya mwisho Kaitaba

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Kaitaba tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar.

Kikosi kimefanya mazoezi kuanzia saa moja usiku kwa kuwa mchezo wetu huo utapigwa muda huo hapa hapa Kaitaba.

Wachezaji wote 24 wameshiriki mazoezi hayo na hakuna ambaye amepata majeraha yatakayomfanya kukosa mchezo wa kesho.

Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Kagera lakini tutapambana kuhakikisha tunapata alama zote tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER