Timu yafanya mazoezi ya mwisho Kaitaba

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Kaitaba kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kesho saa 10 jioni.

Wachezaji wote 21 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Kagera hasa wanapokuwa Kaitaba lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER