Timu yafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuifuata Dodoma Jiji

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kesho kuanza safari ya kuelekea jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Mchezo wetu dhidi ya Dodoma utapigwa Ijumaa katika Uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni.

Kikosi kitaondoka kesho asubuhi kikiwa na wachezaji 20 benchi la ufundi na baadhi ya viongozi tayari kwa mchezo huo.

Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo wetu ili kujihakikishia kumaliza katika nafasi mbili za juu

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER