Timu yafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuifuata De Agosto

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni katika uwanja wetu wa Mo Simba Arena kabla ya kuanza safari ya kuifuata Primiero De Agosto nchini Angola.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo isipokuwa Peter Banda na Shomari Kapombe ambao ni majeruhi ingawa hali zao zinazidi kutengamaa siku hadi siku.

Kikosi kitaondoka kesho saa 10 Alfajiri kikiwa na wachezaji 24 benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.

Mchezo wetu dhidi ya De Agosto utachezwa katika Uwanja wa Novemba 11, Jumapili saa 12 jioni kwa saa za nyumabani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER