Timu yafanya mazoezi ya kwanza Morocco

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya kwanza nchini Morocco yaliyofanyika katika Uwanja Kharma kujiandaa na mchezo wa maruadiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Ijumaa.

Wachezaji wote wamewasili nchini Morocco na wameshiriki mazoezi ya leo kamili kwa mchezo wa Ijumaa ambao tunaamini utakuwa mgumu.

Mazoezi hayo yameanza saa mbili usiku saa za Morocco ambapo nyumbani Tanzania ni saa nne usiku.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anajitahidi kujituma mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kucheza Ijumaa.

Mchezo wetu dhidi ya Wydad utapigwa katika Uwanja wa Mohamed wa V saa moja usiku hapa Morocco ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa tatu usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER