Timu yafanya mazoezi ya kwanza Morocco

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya kwanza katika Uwanja wa Marrakech kujiandaa na mchezo wa Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.

Kikosi kiliwasili katika mji wa Marrakech jana ambapo wachezaji walifanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa ajili ya kuondoa uchovu wa safari lakini leo ndio wameendelea na programu ya mwalimu.

Kesho pia kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja huo huo lakini yatakuwa usiku muda ambao mchezo wetu utapigwa.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kwa asilimia 100 na wanaonekana wapo tayari kuipigania timu kupata ushindi Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER