Timu yafanya mazoezi ya kwanza Malawi

Kikosi chetu kimefanya mazoezi leo jioni katika Uwanja wa ABC Academy kujiandaa na mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets utakaopigwa keshokutwa Jumamosi.

Baada ya kikosi kuwasili hapa Malawi leo saa mbili asubuhi wachezaji na benchi la ufundi walipumzika kabla ya jioni kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili.

Wachezaji wote 25 waliosafiri wamefanya mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri.

Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa wa Bingu ambao utatumika kwa mchezo wa Jumamosi kama kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinavyoelekeza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER