Timu yafanya mazoezi ya kwanza Ivory Coast

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya kwanza nchini Ivory Coast jioni tayari kwa kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Ijumaa saa nne usiku.

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Chuo Cha Polisi (Stade de l’Ecole de Police) na wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki kikamilifu na kila mmoja yupo kwenye hali nzuri.

Baada ya kikosi kufika Ivory Coast jana wachezaji walipewa mapumziko na Leo mchana waliendelea kupumzika kabla ya jioni kuanza mazoezi.

Kesho usiku kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny ambao tutautumia kwa mechi siku ya Ijumaa

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER