Timu yafanya mazoezi ya gym

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya gym asubuhi kwa ajili ya kuweka miili sawa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Yanga utakaopigiwa Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Baada ya mchezo wa juzi kikosi kilifanya mazoezi jana na leo kimeingia gym ili kuwaweka sawa wachezaji.

Jioni kikosi kitaendelea na mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali kutoka kwa benchi la ufundi.

Mchezo wa Jumamosi tumeupa umuhimu mkubwa tunahitaji ushindi ili kutinga fainali na hatimaye tutetee ubingwa wetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER