Timu yafanya mazoezi ya gym chini ya Sbai

Kikosi chetu kimefanya mazoezi asubuhi ya gym chini ya Kocha wa Viungo, Sbai Karim na kisha jioni kama kawaida kitafanya uwanjani.

Kocha Sbai amejiunga na kikosi juzi na tayari ameanza kuwapa mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuwaweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Kikosi kinaendelea kufanya mazoezi kwa awamu mbili asubuhi na jioni huku benchi la ufundi likiridhishwa na viwango vya wachezaji.

Tunatarajia kupata mechi nyingine ya kirafiki katika siku chache zijazo ili kulipa nafasi benchi la ufundi chini ya Kocha Zoran Maki kuwasoma wachezaji jinsi wanavyopokea mafunzo wanayowapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER