Timu yafanya mazoezi ya asubuhi Malawi, kurejea Dar leo

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili leo asubuhi katika Uwanja wa ABC Academy baada ya mchezo wa jana wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets.

Baada ya mazoezi hayo wachezaji watampuzika kwa muda mchache kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam saa saba mchana.

Baada ya kufika Dar es Salaam kikosi kitaanza maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons itakaopigwa Jumatano katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kikosi kinarejea kikiwa na ushindi muhimu wa mabao 2-0 ugenini ambao unatuweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER