Kikosi chetu kimefanya mazoezi usiku huu katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Machi 29.
Kikosi kimewasili hapa Zanzibar jioni ya Leo na wachezaji walipata muda wa kupumzika kwa saa chache kabla ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo kwenye hali nzuri huku wakifuata maelekezo waliyokuwa wakipewa na walimu wao.
Kesho kikosi kitaendelea na programu ya mazoezi ikiwa ni siku ya pili kati ya saba ambazo kitakuwa hapa Zanzibar.