Timu yafanya mazoezi usiku kujiandaa na USGN

Kikosi chetu kimefanya mazoezi usiku huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kujiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie utakaopigwa Jumapili.

Kikosi kimefanya mazoezi muda huu kutokana na mchezo wetu ambao utapigwa saa nne usiku hivyo taratibu za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linataka timu zifanye mazoezi ya mwisho katika wakati wa mechi uliopangwa.

Wachezaji wote isipokuwa Hassan Dilunga ambaye ni majeruhi wamefanya mazoezi na kila mmoja yuko tayari kwa mchezo wa Jumapili.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo na yuko tayari kuipigania timu kuhakikisha tunashinda na kutinga robo fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER