Timu yafanya mazoezi TPC Moshi kujiandaa na Polisi

Kikosi chetu kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Limpopo TPC Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania.

Kikosi kimewasili Moshi saa 10 jioni kutoka jijini Tanga na saa 12 kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili baada ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union.

Wachezaji wote waliosafiri wamefanya mazoezi na hakuna aliyepata maumivu kwenye mchezo wetu wa jana.

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Ushirika ambao utatumika kwenye mchezo wetu Jumapili saa 10 jioni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER