Timu yafanya mazoezi mwisho kujiandaa na Mlandege Kesho

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kujiandaa na mchezo wa kesho wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege utakaofanyika saa 2:15 usiku.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yoyote aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Kikosi kipo tayari kwa mchezo huo ambao tunatarajia utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na lengo moja tu la kuhakikisha tunashinda na kuchukua ubingwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER