Timu yafanya mazoezi Mo Arena

Baada ya kuingia rasmi kambini leo mchana kikosi kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie ya Niger

Wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya michuano hii wameingia kambini na jioni wamefanya mazoezi tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ambao tunauchukulia kama fainali.

Morali ya wachezaji ipo juu na wameahidi kuhakikisha wanajitoa wakati wote wa mchezo ili kupata ushindi ambao utatupa tiketi ya kutinga robo fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER