Timu yafanya mazoezi mepesi Nyamagana

Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi mepesi ya utimamu wa mwili katika Uwanja wa Nyamagana baada ya kurejea kutoka mkoani Kagera.

Kikosi kimefika jijini Mwanza jana jioni na wachezaji wakapewa mapumziko kabla ya kuanza mazoezi mepesi leo jioni.

Moses Phiri ndiye mchezaji pekee ambaye hajashiriki mazoezi hayo baada ya kupata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera.

Kesho kikosi kitaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC utakaopigwa Jumatatu katika Uwanja wa CCM Kirumba

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER