Timu yafanya mazoezi Dar, kuifuata Coastal Tanga leo

Kikosi chetu kimefanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi katika dimba la Mkwakwani.

Baada ya mazoezi hayo mchana kikosi kitaanza safari ya kuelekea Tanga tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi ya asubuhi na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Tanga.

Tunafahamu moja ya viwanja vigumu kupata pointi tatu ni Mkwakwani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapambana kuhakikisha tunaondoka na alama zote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER