Timu yaendelea na mazoezi Uturuki

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano hapa Ankara, Uturuki ikiwa leo ni siku ya tano.

Kama kawaida programu ya mazoezi ilikuwa ya awamu mbili asubuhi na jioni. Asubuhi mazoezi yalikuwa ya nguvu zaidi na jioni yakiwa ya kucheza mpira uwanjani.

Baada ya mazoezi ya jioni wachezaji walitakiwa kuingia kwenye eneo maalumu lililokuwa na maji yenye barafu kwa ajili ya kuweka miili sawa (recovery) baada ya kufanya mazoezi magumu.

Meneja na Mtaalamu wa Sayansi ya Michezo, Mikael Igendia amesema umuhimu wa kuwaweka wachezaji kwenye maji yaliyochanganywa na baarafu ni kuweka miili sawa sababu wanafanya mazoezi magumu muda mwingi na nguvu kubwa inatumika.

“Mazoezi ya siku mbili hizi yamekuwa magumu na wachezaji wametumia nguvu nyingi kwahiyo kuingia kwenye maji yenye barafu miili yao itarudi kwenye hali ya kawaida na kesho wataweza kuendelea na ratiba nyingine.”

“Bila ya kufanya hivi wachezaji miili yao ingekuwa imechoka zaidi na hata katika programu zetu nyingine wasingeweza kufanya kama tunavyohitaji,” amesema Igendia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER