Timu yaendelea na mazoezi Mo Arena kujiandaa na Ihefu

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Ihefu FC yaliyofanyika kwenye Uwanja wetu wa Mo Simba Arena.

Mazoezi hayo yamesimamiwa na kocha mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akisaidiana na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.

Mchezaji pekee ambaye amekosekana kwenye mazoezi ya leo ni mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe ambaye amepewa mapumziko ya wiki moja kutokana na kupata maumivu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Wachezaji, Augustine Okrah, Ismael Sawadogo na Peter Banda ambao walikuwa majeruhi wote wamerejea na wameshiriki mazoezi hayo.

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho jioni kwakuwa mchezo wetu wa Ijumaa utakaopigwa Uwanja wa Uhuru utafanyika muda huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER