Timu yaendelea na Mazoezi Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Ijumaa.

Mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Ijumaa saa moja usiku.

Timu ilianza mazoezi jana baada ya kurejea juzi kutoka mkoani Mtwara ilipocheza nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa kuipigania timu kuhakikisha tunapata pointi tatu siku ya Ijumaa.

Kwa sasa malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu tatu za ligi zilizosalia tukianza na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER