Timu yaendelea kujifua Mo Arena

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi kwenye dimba la Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Wachezaji wote isipokuwa Hassan Dilunga ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu wamefanya mazoezi tayari kwa mchezo huo mkubwa unaosubiriwa kwa hamu.

Aidha, nyota Clatous Chama na Bernard Morrison ambao hawakwenda Afrika Kusini katika mchezo wa mwisho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates nao wamejumuika mazoezini.

Kwa sasa tunaangalia jinsi ya kushinda mechi zetu 11 za ligi zilizobaki pamoja na Michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kutolewa kimataifa.

Kila mchezo ulio mbele yetu utakuwa kama fainali kwakuwa tunataka kumaliza vizuri msimu wa ligi 2021/22.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER