Timu yaendelea kujifua Mo Arena

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Primiero De Agosto utakaopigwa Jumapili Luanda, nchini Angola.

Kikosi kimeingia rasmi kambini jana kujiandaa na mchezo huo ambao tunahitaji kupata matokeo mazuri ugenini ili mechi ya marudio nyumbani isiwe ya presha kwetu.

Wachezaji Pape Sakho ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia na Henock Inonga aliyepata maumivu kabla ya mchezo wetu dhidi Dodoma Jiji wapo vizuri na tayari wamejiunga na wenzao kuunda kambi hiyo.

Wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ipo juu kuelekea mchezo huo ambapo kama tukifanikiwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote mbili tutaingia kwenye hatua ya makundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER