Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wetu wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Baada ya mchezo wa Simba Day dhidi ya St. George wachezaji walirudi mazoezini tayari kwa kujiandaa na mchezo huo muhimu ambao tunahitaji ushindi.
Kesho, kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho asubuhi katika Uwanja wa Mo Arena ili kuwaweka tayari kwa mchezo wa Jumamosi.
Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yeyote ambaye amepata maumivu yatakayomfanya akose mchezo.