Timu yaanza safari ya kurudi nyumbani

Kikosi chetu kimeanza safari ya kurejea nyumbani baada ya sare ya bila kufungana tuliopata juzi dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny.

Kikosi kitapitia Ethiopia kabla ya kuanza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam na kinatarajia kuwasili saa tisa alfajiri.

Baada ya kufika timu itaanza maandalizi ya mchezo wa hatua ya 32 bora ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya TRA utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex, Februari saa moja usiku.

Machi 2 tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Jwaneng Galaxy kutoka Botswana kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER