Kikosi chetu kimeondoka Libya kuelekea nchini Uturuki tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Al Ahli Tripoli.
Baada ya kufika Uturuki timu itabadili Ndege kuja Tanzania na inatarajia kuwasili nchini saa tisa alfajiri.
Kikosi kikiwasili kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa Jumapili saa 10 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa.