Timu yaanza safari kurejea nyumbani, kutua Dar kesho mchana

Kikosi chetu kimeanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kumaliza mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane uliopigwa usiku wa kuamkia leo.

Timu imeondoka Mjini Oujda kuelekea Casablanca ambapo mchana huu watapanda ndege hadi Dubai na kuunganisha ndege hadi Dar es Salaam ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) saa saba mchana.

Meneja wa timu Patrick Rweyemamu, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeraha yalipoatikana katika mchezo wa jana dhidi ya Barkane.

“Tumeanza safari ya kurejea nyumbani na tunatarajia kufika kesho mchana. Tunashukuru wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna ambaye amepata majeraha kwenye mchezo wa jana. Tukifika tu maandalizi ya mechi za ligi yanaanza,” amesema Rweyemamu.

Baada ya kuwasili kikosi kitaanza moja kwa moja maandalizi ya mechi mbili za Ligi kuu ya NBC dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji kabla ya kushuka tena dimbani kurudiana na Barkane Machi 13, mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER