Timu yaanza mazoezi Zanzibar

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya kwanza Visiwani Zanzibar tayari kwa kujiandaa na mechi zetu za Ligi Kuu ya NBC zilizosalia.

Kikosi kimewasili hapa Zanzibar saa tisa Alasiri na hii jioni kimefanya mazoezi katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex.

Wachezaji wote 28 wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kuendelea kujifua kwa ajili ya mechi hizo.

Kikosi kitaendelea na programu ya mazoezi hapa Visiwani Zanzibar kwa siku mbili zijazo kabla ya kurejea Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER