Timu yaanza mazoezi kujiwinda na ASEC

Kikosi chetu kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 25.

Wachezaji wameanza na mazoezi ya gym huku wale walioitwa timu za taifa wakiruhisiwa kwenda kujiunga nazo.

Baada ya mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Namungo wachezaji walipewa mapumziko mafupi kabla ya leo kuanza mazoezi ya gym.

Mazoezi ya gym ni kwa ajili ya kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji kabla ya kuelekea uwanjani kujifunza mbinu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER