Timu ya vijana yaichapa Ihefu Azam Complex

Timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 20 imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ihefu katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nane bora ya Ligi uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku tukilisakama zaidi lango la mpinzani na wao wakijibu mapigo kwa mashambulizi ya kushtukiza.

Pamoja na mashambulizi mengi ya pande zote lakini katika dakika 45 za kipindi cha kwanza hakuna timu iliyopata bao.

Kipindi cha pili tulianza kwa kasi na kuwashambulia Ihefu na dakika ya 63 tulipata bao la kwanza lililofungwa na Razak Bashir kwa mpira wa kona ambayo ilingia moja kwa moja wavuni

Dakika tano baadaye tuliendelea kuwashambulia na kuzidi kuwapa presha na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Juma Ali.

Baada ya ushindi wa leo kikosi chetu cha vijana kitashuka tena uwanjani Jumatano katika mchezo wa pili wa kundi A.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER