Timu kwenda Uturuki kwa kambi ya wiki tatu

Kikosi chetu kinatarajia kutaondoka nchini muda wowote kutoka sasa kuelekea Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya wa Ligi 2023/24.

Timu itaondoka na kikosi kamili tulichokisajili kwa msimu ujao wa ligi chini ya kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na benchi zima la ufundi.

Wachezaji wapya tuliowaasjili wa ndani na wale wa kimataifa nao watakuwa sehemu ya kambi hiyo nchini Uturuki.

Kambi ya Uturuki ni mapendekezo ya benchi la ufundi ambao wanaamini wachezaji watapata utulivu na kuyashika mafundisho watakayopewa.

Kikiwa nchini Uturuki tunategemea kikosi chetu kitapata mechi kadhaa za kirafiki ili benchi la ufundi lijue mapokeo ya mafunzo wanayowapa nyota wetu kabla ya kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER