Timu kurudi mazoezini kesho kujiandaa na Dodoma Jiji

Kikosi chetu kesho asubuhi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Baada ya ushindi wa jana mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja kwenda na kesho wachezaji watarejea mazoezini.

Wachezaji wapya tuliowasajili katika dirisha hili Hamed Ismael Sawadogo, Jean Baleke na Mohamed Mussa watashiriki mazoezi ya kesho.

Kama Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake wataona inafaa wanaweza kuwatumia katika mchezo huo kwa kuwa masuala yao ya vibali tayari yamekamilika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER