Kikosi cha wachezaji tisa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kitaanza mazoezi kesho Jumapili kujiweka sawa baada ya mapumziko ya siku chache baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrikh.
Timu itaanza mazoezi ikiwa na nyota hao tisa kutokana na wachezaji 18 kuitwa kwenye timu zao za taifa huku 10 wakiitwa kwenye kikosi cha Tanzania ‘Taifa Stars’ na wengine wakiwa wachezaji wa Kimataifa.
Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema Kocha, Didier Gomez ameamua kufanya mazoezi na timu ya vijana ili kuwapa mazoezi nyota wake tisa waliobaki kikosini.
“Kikosi kitarejea mazoezini kesho Jumapili na kitakuwa pamoja na timu ya vijana kwa kuwa tumebaki na wachezaji tisa kikosini sababu wengine 18 wameitwa katika timu zao za taifa,” amesema Rweyemamu.
Kocha Gomez anaandaa kikosi kwa ajili ya mchezo ujao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa Aprili 2, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
3 Responses
Mandalizi mema timu yngu
Ahsanteni kwa taarifa nzuri ila tunaomba muweke na utaratibu wa kuuza bidhaa za klabu online
Kila LA kheri na point tatu muhimu kwa chama langu