Kikosi chetu leo jioni kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco utakaopigwa Jumamosi saa nne usiku nchini Morocco.
Wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Botswana usiku wa kumkia jana tulipokuwa na mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Wachezaji wote isipokuwa majeruhi wanatarajia kushiriki mazoezi ya leo chini ya Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha na wasaidizi wake.
Baada ya mazoezi ya jioni kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kuendelea na maandalizi ya mchezo huo.