Timu kurejea mazoezini kesho kujiandaa na Namungo

Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kuahirishwa wachezaji walipewa mapumziko mafupi na kesho kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata.

Mchezo dhidi ya Dodoma ulipangwa kufanyika Jumamosi, Februari 15 lakini wenzetu walipata ajali hivyo Bodi ya Ligi ilitangaza jana kuwa mchezo huo umeahirishwa.

Mechi yetu inayofuata itakuwa dhidi ya Namungo FC ambayo itapigwa katika Uwanja wa Majaliwa, Februari 19 siku ya Jumatano saa 12:30 jioni.

Wachezaji wote watarejea kesho na moja kwa moja wataanza maandalizi ya mchezo huo ambao malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER