Timu kurejea kesho mchana

Kikosi chetu kitarejea nchini kesho saa sita mchana kutoka Benin baada ya kumaliza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.

Timu itaondoka mchana Benin ambapo italala Ethiopia na kesho asubuhi itaanza safari ya kurejea nchini.

Baada ya kutua jijini Dar es Salaam wachezaji walioitwa timu za taifa wataruhisiwa kwenda kujiunga nazo wakati wale wengine watapewa mapumziko mafupi.

Wachezaji ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa watarejea mazoezini mapema kufanya maandalizi ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya US Gendarmerie utakaopigiwa Aprili 3, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER