Timu kupumzika Uturuki, kupaa Morocco kesho

Kikosi chetu kitaendelea kubaki jijini Istanbul Uturuki hadi kesho saa tano asubuhi kitapoanza safari ya kuelekea Casablanca Morocco kwa ajili ya kambi fupi ya maandalizi.

Kikosi kiliwasili jana usiku hapa Istanbul kutoka nchini Niger baada ya mchezo wetu dhidi ya US Gendarmerie na kimepata mapumziko kabla ya kuanza safari kesho.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kikosi kiko katika hali nzuri na kila kitu kinaenda sawa kuelekea safari ya kuelekea Morocco.

“Tumefika salama hapa Istanbul jana usiku, leo tumepumzika na kesho saa tano asubuhi tutaanza safari ya kuelekea Morocco.

“Baada ya kufika jijini Casablanca tutaweka kambi ya siku nne kabla ya kwenda Berkane tayari kwa mchezo wetu wa tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopogwa Jumapili,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER