Kikosi chetu kinatarajia kuondoka nchini Jumamosi alfajiri Oktoba 8, kuekekea Angola tayari kwa mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CD Primeiro De Agosto.
Kikosi kitaondoka kwa ndege maalumu ya kukodi itakayobeba wachezaji, benchi la ufundi viongozi na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini.
Baada ya ushindi dhidi ya Dodoma Jiji tayari kikosi kimerejea mazoezini jana kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Oktoba 9, katika dimba la Novemba 11.
Kuelekea mchezo huo tutaendelea kuwakosa wachezaji Shomari Kapombe, Peter Banda na Jimyson Mwanuke ambao ni majeruhi
Wakati huo huo, Pape Osman Sakho ameshajiunga na kikosi baada ya kukosekana katika mchezo dhidi ya Dodoma baada kusafiri kwenda Senegal kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.
Kwa upande wake mlinzi wa kati, Henock Inonga anaendelea vema baada ya juzi kupata hitilafu kiafya saa chache kabla ya kuanza mchezo dhidi ya Dodoma.