Timu kupaa alfajiri kuelekea Sudan

Kikosi chetu kitaondoka kesho saa 10 Alfajiri kuelekea Khartoum, Sudan tayari kwa mechi mbili za kirafiki za kimataifa baada ya kupata mwaliko maalumu kutoka kwa Al Hilal.

Kikosi kitaondoka kikiwa na msafara wa watu 30 wachezaji wakiwa 20 benchi la ufundi na Viongozi wachache.

Meneja wa Timu Patrick Rweyemamu, amesema kikosi kinatarajia kufika jijini Khartoum kesho saa tano asubuhi na kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili jioni.

“Kama tulivyotangaza awali tumepokea mwaliko kutoka kwa wenzetu Al Hilal na kesho saa 10 alfajiri tutaanza safari ya kuelekea Sudan tukiwa na msafara wa watu 30 na tutafika jijini Khartoum kesho.

“Baada ya kikosi kuwasili Sudan wachezaji watapumzika kwa saa chache kabla ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili na Jumamosi tutafanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo,” amesema Rweyemamu.

Kikosi chetu kitacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana, Agosti 28 na siku tatu baadaye tutacheza na wenyeji Al Hilal.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER