Timu kuondoka usiku kuelekea Berkane

Kikosi chetu kinatarajia kuondoka usiku jijini Casablanca kuelekea Mji wa Berkane tayari kwa mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane Jumapili.

Meneja wa timu Patrick Rweyemamu amesema baada ya kuondoka Casablanca kikosi kitapumzika na kesho asubuhi kitaanza safari ya kuelekea Berkane.

Rweyemamu ameongeza kuwa kikosi kikifika Berkane kitafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani Jumapili.

“Baada ya mazoezi ya leo jioni kikosi kitapumzika kidogo kabla ya kuanza safari ya kuelekea Berkane. Tukifika kule tutafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa kabla ya mchezo,” amesema Rweyemamu.

Akizungumzia hali ya kikosi, Rweyemamu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri isipokuwa kuna uwezekano kiungo Jonas Mkude akaendelea kukosekana kutokana na afya yake kutotengamaa.

“Tumesafiri na wachezaji 23 lakini Clatous Chama hatacheza kwa sababu alishatumikia timu nyingine hatua iliyopita. Mkude yeye yupo chini ya uangalizi ingawa ameanza mazoezi lakini sina uhakika kama atakuwa tayari kwa mchezo wa Jumapili,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER