Kesho saa sita mchana kikosi chetu kitasafiri kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumapili.
Mchezo wetu dhidi ya Kagera ambao tunatarajia utakuwa mgumu kutokana na ubora walionao wapinzani utapigwa Jumapili saa 10 jioni katika Uwanja Kaitaba.
Timu itaondoka na kikosi cha wachezaji 21 ambao tunaamini wataweza kutupatia ushindi kwenye mchezo wa Jumapili.
Kwa sasa malengo ya timu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo uliopo mbele yetu ili kuendelea kukaa juu kwenye msimamo wa Ligi.