Timu kuondoka mchana kuelekea Mtwara

Kikosi chetu kitaondoka muda mfupi ujao kutoka hapa Ruangwa kuelekea Mtwara tayari kwa mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kabla ya kuondoka Ruangwa kikosi kimefanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa Majaliwa ili kuwaweka sawa wachezaji.

Wachezaji wote waliopo kikosini wapo kwenye hali nzuri tayari kupambania timu kufanya vizuri ili tutinge fainali ya michuano hiyo.

Morali za wachezaji zipo juu kuanzia uwanja wa mazoezi, wanapokuwa wamepumzika au wakati wa kula wanazungumza kuelekea mchezo huo.

Mchezo wetu dhidi ya Azam utapigwa Nangwanda Jumapili kuanzia saa 9:30 Alasiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER