Timu Kuondoka Kesho jioni kuifuata Vipers

Kikosi cha wachezaji 25 benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi kitaondoka kesho jioni kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi dhidi ya Vipers.

Kabla ya kuondoka kikosi kitafanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena ili kuwaweka sawa wachezaji.

Tumeamua kuondoka na kikosi kamili kwakuwa tunaenda Uganda tukiwa na lengo la kuhitaji ushindi.

Ushindi katika mchezo dhidi ya Vipers utarejesha matumaini yetu ya kuvuka hatua hii ya makundi ndio maana tumechukua tahadhari zote.

Mchezo dhidi ya Vipers utapigwa katika Uwanja wa St. Mary’s wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15000 Jumamosi Februari 26, saa moja usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER