Timu kuondoka jioni kuifuata Singida Big Stars

Kikosi chetu kitaondoka leo saa 10 jioni kuelekea Dodoma kwa ndege kabla ya kuunganisha kwa basi hadi mkoani Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Singida Big Stars utakaopigiwa Jumatano Uwanja wa Liti.

Timu itaondoka na wachezaji 22 tayari kwa mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu.

Kabla ya kuondoka leo asubuhi kikosi kimefanya mazoezi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kuwaweka sawa wachezaji kabla ya kuanza safari.

Kikosi kilianza mazoezi wiki moja iliyopita na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu muhimu ugenini.

Tutashuka katika mchezo huo tukijua utakuwa mgumu na tunawaheshimu Singida lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER