Kikosi cha wachezaji 21 kitaondoka jioni kuelekea jijini Dodoma tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Jumapili, Uwanja wa Jamhuri.
Baada ya kuwasili jijini Dodoma, kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho kabla ya kushuka dimbani Jumapili kuikabili Dodoma.
Tunasafiri tukiwa tunajua tunaenda kukutana na timu bora katika uwanja wa ugenini, tunaiheshimu Dodoma na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kupambana kupata pointi tatu.
Kwa sasa ligi ipo mzunguko wa pili na kila timu inapambana kutafuta pointi tatu ili kujiweka nafasi nzuri nasi tumejipanga na kila mchezo tumeupa umuhimu sawa.