Timu Kuondoka asubuhi kuelekea Kigoma

Kikosi chetu kitaondoka jijini Dar es Salaam saa tano asubuhi kuelekea mkoani Kigoma tayari kwa mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika saa 10 jioni.

Kikosi kitaondoka na jumla ya wachezaji 23 tayari kwa mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wetu Mashujaa kuwa katika nafasi ambayo sio nzuri kwenye msimamo.

Katika mchezo wa jana tulioibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tembo FC kutoka Tabora hatukupata majeruhi yoyote ambaye tutamkosa katika mechi ya Jumamosi.

Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho katika Uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuivaa Mashujaa Jumamosi.

Licha ya kufahamu utakuwa mchezo mgumu lakini tutaingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha tunashinda na kuondoka na pointi zote tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER