Timu Kuingia Kambini Leo kujiandaa na Vipers

Baada ya mazoezi ya leo jioni kikosi chetu kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumanne, Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni siku tano kabla ya mechi husika kwakuwa tunahitaji kupata ushindi.

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema lengo letu ni moja kuhakikisha tunashinda mchezo hivyo tunapaswa kujipanga vizuri.

Ahmed amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwachanganya Vipers ambao hawajawahi kukutana na shangwe la Wanasimba wakiwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

“Baada ya mchezo wa jana wa FA dhidi ya African Sports, leo kikosi kinaingia kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Vipers.

“Kikubwa tunaendelea kuwasisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwapa sapoti wachezaji wetu, kule Uganda tulikuwa wachache lakini Jumanne tutakuwa wote na shangwe itakuwa kubwa,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER