Timu kuingia kambini Kujiandaa na Singida Big Stars

Kikosi chetu leo kitaingia kambini baada ya mazoezi ya jioni kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Ijumaa saa moja usiku.

Baada ya mchezo wa hatua ya tatu ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Coastal Union juzi wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi wakitokea nyumbani lakini leo wanaingia kambini rasmi.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri na kikosi kitaingia kambini baada ya mazoezi ya jioni.

“Kikosi kitaingia kambini baada ya mazoezi ya jioni. Wachezaji walikuwa wanatokea nyumbani baada ya mchezo dhidi ya Coastal lakini leo tunaingia kambini kujiandaa na Singida.

“Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Liti tulitoka sare sasa tunataka kuwauliza ile sare waliipataje,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER