Timu Kuingia Kambini Kujiandaa na De Agosto

Kikosi chetu leo kitaingia kambini baada ya mazoezi ya jioni kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto utakaofanyika Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Baada ya mapumziko ya siku moja waliopewa wachezaji waliporudi kutoka Angola jana walianza mazoezi na leo jioni wataingia kambini moja kwa moja.

Wachezaji wote 24 ambao tulisafiri nao kwenda Angola wapo kwenye hali nzuri na jana wamefanya mazoezi na wataingia kambini.

Tumejipanga kuingia katika mchezo wa Jumapili bila kuangalia matokeo mazuri ya mechi ya kwanza, hatutaki sababu yoyote itufanye tukose kufuzu hatua ya makundi.

Tayari viingilio vya mchezo vimetangazwa na vituo zinapotikana pia vimewekwa hadharani ili mashabiki wanunue mapema kuepusha usumbufu siku ya mechi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER