Timu kuingia Kambini Kesho kujiandaa dhidi ya Yanga

Kikosi chetu kitaingia kambini kesho kuanza maandalizi ya mchezo wa mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kwa kawaida timu huingia kambini siku tatu kabla ya mchezo lakini sasa imeingia siku tano kabla kutokana na ukubwa wa umuhimu wa mechi.

Ahmed amesema licha ya ubora walionao watani wetu kwa sasa lakini tutaingia kwenye mchezo huo kwa lengo la kutafuta pointi tatu.

“Timu itaingia kambini kesho tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa Derby dhidi ya Yanga, bila kujalisha chochote tutaingia kwa lengo la kutafuta pointi tatu na kuwapa furaha Wanasimba,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER